Swali: Picha zinazokuwa kwenye TV zinafaa?

Jibu: Ni haramu; ni mamoja kwenye TV au kwenginepo.

Swali: Vipi picha zinazokuwa kwenye msikiti Mtukufu wa Makkah?

Jibu: Picha zipi? Hii sio picha. Wanarusha moja kwa moja bila picha. Sio kitu kinachobaki. Wanarusha moja kwa moja swalah kwenye runinga. Hii sio picha yenye kubaki. Ni kama vile kioo kilichowekwa na watu wanaweza kukiona.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22670/حكم-التصوير-في-التلفزيون-والحرم-ونحوه
  • Imechapishwa: 15/07/2023