374 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

ثلاثٌ أحلِفُ عليهنَّ: لا يجعلُ الله مَن له سهمٌ في الإسلامِ كمَن لا سَهمَ له، وأسهمُ الإسلامِ ثلاثةٌ: الصلاةُ، والصومُ، والزكاة، ولا يَتَوَلَّى اللهُ عبداً في الدنيا؛ فَيُولِّيَه غيرَه يومَ القيامةِ، ولا يحب رجلٌ قوماً؛ إلاّ جعلَه الله معهم، والرابعةُ لو حلفتُ عليها رَجَوتُ أن لا آثمَ: لا يستُرُ الله عبداً في الدنيا؛ إلا سَتَرَه يومَ القيامةِ

“Naapa juu ya mambo matatu: Allaah hatomfanya yule mwenye fungu kuwa sawa na asiyekuwa na fungu. Mafungu ya Uislamu ni matatu: swalah, swawm na zakaah. Allaah hatomsimamia mja duniani ambapo akawepo mwingine wa kumsimamia siku ya Qiyaamah. Hakuna mtu atakayewapenda watu isipokuwa Allaah atamfanya kuwa pamoja nao. Ikiwa nitaapia jambo la nne, basi nataraji kuwa sintokuwa nimetenda dhambi; Allaah hatomsitiri mja duniani isipokuwa atamsitiri pia siku ya Qiyaamah.”[1]

Ameipokea Ahmad kwa cheni ya wapokezi nzuri.

375 – at-Twabaraaniy ameipokea katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” kupitia kwa Ibn Mas´uud[2].

[1] Swahiyh kupitia zingine.

[2] Swahiyh kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/273-274)
  • Imechapishwa: 31/08/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy