23. Bora msafiri akusanye wakati wa mwanzo au wakati wa pili?

Swali 23: Bora ni kukusanya katika ule wakati wa swalah ya kwanza au ule wakati wa swalah ya pili nikiwa msafiri na nataka kukusanya[1]?

Jibu: Bora ni wewe kufanya lile jepesi zaidi kwako na kwa marafiki zako. Ukiwa ni mkazi ukazi ambao hauzuii kufupisha wala kukusanya, basi bora ni kuacha kufanya hivo. Kwa njia ya kwamba wewe na marafiki zako mkaswali kila swalah ndani ya wakati wake. Hivo ndivo alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika hajj ya kuaga alipokuwa Minaa. Lakini ukiwa ni mwenye kuendelea na safari bora ni wewe kukusanya katika ule wakati wa swalah ya kwanza. Ukiwa umeanza safari kabla ya kuingia wakati wa swalah ya kwanza basi bora ni wewe kukusanya katika ule wakati wa swalah ya pili. Kwa sababu imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka katika Hadiyth ya Anas na wengineo yanayojulisha juu ya hayo.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa, uk. 474

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 38-39
  • Imechapishwa: 07/03/2022