24. Wakati wa kukusanya kati ya swalah mbili na wakati wa Witr

Swali 24: Ni upi wakati wa kukusanya kati ya swalah mbili na ni upi wakati wa Witr[1]?

Jibu: Kukusanya kati ya swalah mbili kunakuwa katika ule wakati wa [swalah ya] kwanza au ya mwisho. Wigo ni mpana katika jambo la kukusanya. Shari´ah takasifu imejulisha juu ya kufaa kwake katika wakati wa ya kwanza na ya pili au kati yazo. Kwa sababu wakati wazo umekuwa wakati mmoja kwa ambaye amepewa udhuru kama mfano wa msafiri na mgonjwa. Vilevile inafaa kuongea kati ya swalah hizo mbili zilizokusanywa kwa yale yanayohitajika.

Kuhusu Witr wakati wake unaanza kuanzia pale mtu anapomaliza kuswali ´Ishaa ijapo imekusanywa pamoja na Maghrib katika wakati wa swalah ya Maghrib. Wakati wake unamalizika kwa kuchomoza kwa Fajr.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/282).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 39-40
  • Imechapishwa: 07/03/2022