22. Tawhiyd waliyolingania Mitume na washirikina wakaikataa

hapo ndipo utajua Tawhiyd waliyoilingania kwayo Mitume na washirikina wakakataa kuikubali.

MAELEZO

Ukielewa zile Aayah zilizotangulia zilizo wazi zinazothibitisha kuwa washirikina wa mwanzo hawakushirikisha katika uola, bali walishirikisha katika uungu ambapo walijichukulia waungu badala ya Allaah ili wawakurubishe kwa Allaah (´Azza wa Jall) na wawaombee mbele Yake, ndipo utatambua kuwa Tawhiyd ambayo Mitume walilingania kwayo na washirikina wakaikanusha ni Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah na sio Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah na kwamba kukubali Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah peke yake hakutoshelezi na hakumwingizi yule aliyeikubali katika Uislamu. Tambua hili ni jambo muhimu sana kwa kuwa ndipo mtu atajua Tawhiyd na shirki, Uislamu na kufuru. Kutojua hilo madhara yake ni makubwa na khatari yake ni kuu kwa kuwa mtu anaweza kutoka katika Uislamu pasi na kujua.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 37
  • Imechapishwa: 06/11/2016