Uislamu unalingania pia katika udugu wa kiimani, kunasihi kwa ajili ya Allaah na waja Wake na muislamu kumuheshimu ndugu yake. Asimfanyie dhuluma, husuda, ghushi, khiyana na mengineyo katika maadili mabaya. Amesema (Jalla wa ´Alaa):

وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ

“Waumini wanaume na waumini wanawake ni marafiki wao kwa wao.”[1]

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ

“Hakika si vyenginevyo waumini ni ndugu.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Muislamu ni ndugu wa muislamu mwenzie; hamdhulumu, hamdharau, hamtosi…”[3]

Muislamu ni nduguye muislamu. Ni lazima kwake kumuheshimu na asimdharau. Vilevile ni lazima kumfanyia uadilifu na kumpa haki yake kwa nyanja zote zilizowekwa katika Shari´ah na Allaah. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Muumini kwa muumini mwenziwe ni kama jengo; upande mmoja unaupa nguvu upande mwingine.”[4]

“Muumini ni kioo cha ndugu yake muumini.”[5]

Wewe, ndugu yangu, ni kioo cha ndugu yako. Wewe ni moja katika majengo ambayo kumesimama juu udugu wa kiimani. Kwa hivyo mche Allaah juu ya haki ya ndugu yako na itambue haki yake. Tangamana naye kwa haki, ushauri na ukweli.

[1] 09:71

[2] 49:10

[3] Muslim (2442) na Muslim (2580).

[4] al-Bukhaariy (481) na Muslim (2585).

[5] Abu Daawuud (4272).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Da´wah ilaa Allaah wa Akhlaaq-id-Du´aah, uk. 36
  • Imechapishwa: 14/06/2023