Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya matarajio ni Kauli Yake (Ta´ala):

فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا

“Hivyo anayetaraji kukutana na Mola wake na atende ‘amali njema na wala asishirikishe katika ‘ibaadah za Mola wake yeyote.” (al-Kahf 18 : 110)

MAELEZO

Kutaraji ni ´ibaadah. Mtu anatakiwa kumtarajia Allaah na kuwa na dhana njema Kwake. Amesema (Ta´ala):

فَمَن كَانَ يَرْجُو لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا

“Hivyo anayetaraji kukutana na Mola wake na atende ‘amali njema na wala asishirikishe katika ‘ibaadah za Mola wake yeyote.” (18:110)

Kuyatia matarajio Kwake na kuwa na matumaini kwa vilivyoko Kwake (Subhaanahu wa Ta´ala) ni ´ibaadah. Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ

“Hakika wao walikuwa wakikimbilia katika mambo ya kheri na wakituomba kwa matumaini na khofu na walikuwa Kwetu wenye kunyenyekea.” (21:90)

Matumaini ni matarajio na woga ni khofu. Vyote viwili ni ´ibaadah. Mja anatakiwa kumjengea Mola wake dhana nzuri na afanye sababu za Kishari´ah. Kumjengea Allaah dhana nzuri pamoja na kufanya sababu za Kishari´ah kunamletea mja matunda mazuri pamoja na kurehemewa, kuingia Peponi na kusamehewa madhambi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 34-35
  • Imechapishwa: 12/12/2016