21. Hadiyth “Yule mwenye kutawadha na kuswali kama alivyoamrishwa… “

196 – Abu Ayyuub ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

مَن توضّأَ كما أُمِرَ، وصلى كما أُمِرَ؛ غُفِرَ له ما قدَّم من عمل

“Yule mwenye kutawadha na kuswali kama alivyoamrishwa, basi atasamehewa matendo yake yaliyotangulia.”[1]

Ameipokea an-Nasaa´iy, Ibn Maajah na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake kwa tamko lisemalo:

مَن توضّأَ كما أُمِرَ غُفِرَ له ما تقدَّمَ من ذنبه

“Yule mwenye kutawadha kama alivyoamrishwa, basi atasamehewa dhambi zake zilizotangulia.”

[1] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/197)
  • Imechapishwa: 29/12/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy