Abu Muhammad ´Abdur-Rahmaan bin Abiy Haatim amesema:
4 – Mtu bora wa Ummah huu baada ya Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Abu Bakr as-Swiddiyq, ´Umar bin al-Khattwaab, ´Uthmaan bin ´Affaan na ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anhum). Wao ndio makhaliyfah waongofu na wenye kuongoza.
MAELEZO
Miongoni mwa ´Aqiydah na misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kuwaheshimu Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kuwapenda na kuitakidi kuwa wao ni bora kuliko ummah mzima walobaki. Allaah awawie radhi! Ibn Abiy Haatim amesema:
“Mtu bora wa Ummah huu baada ya Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Abu Bakr asw-Swiddiyq… “
Ahl-us-Sunnah hawana shaka juu ya hili. Hata Khawaarij vilevile wanaitakidi kuwa Abu Bakr na ´Umar ndio bora, wanamchukia ´Uthmaan, ´Aliy na wengine. Ahl-us-Sunnah ni wenye kuzunguka na haki na dalili – himdi zote anastahiki Allaah. Wanajua ni hadhi gani walionayo Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanatambua kuwa wanatofautiana katika fadhila na kwamba baadhi ni bora kuliko wengine, kama ilivyosihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
- Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qurrat-ul-´Aynayn bi Tawdhwiyh Ma´aaniy ´Aqiydat-ir-Raaziyayn, uk. 34-35
- Imechapishwa: 15/10/2016
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)