20. Allaah anafanya akitakacho na hakuna yeyote wa kupingana Naye

Kwa hali yoyote Ahl-us-Sunnah wanaamini Qadar kwa njia ifuatayo:

1- Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ameyajua mambo yote kabla ya kutokea kwake. Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) amejua muda wa viumbe kueshi, riziki, matendo yao na kila kitu.

2- Akayaandika kwenye ubao Uliohifadhiwa.

3- Yakaandikwa tena pindi kipomoko kinapopuliziwa roho tumboni.

4- Matakwa ya Allaah ni yenye kukienea kila kitu na hakuna kinachoyaeupuka. Hakuna kitu kinachokuwa katika ulimwengu huu isipokuwa kile alichokitaka Allaah (Subhaanahu wa Ta´al).

Pamoja na hivyo waja ni wenye jukumu juu ya matendo yao; ni wenye kuamrishwa na kukatazwa. Allaah amewaumba ili wamuabudu na ili awaamrishe na kuwakataza:

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ

” Sikuumba majini na wanadamu isipokuwa waniabudu.” 51:56

Atawafanyia hesabu makafiri, atawaingiza Motoni na kuwadumisha humo milele kwa ajili ya matendo yao waliyoyafanya kwa khiyari yao. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anawaongoza watu wema na waumini katika matendo mema na yanayotakikana. Makafiri hakuwafanya hivo. Hii ni haki na fadhila Zake. Akitaka anawapa na akitaka anaacha kufanya hivo. Amewaacha makafiri hao juu ya nafsi zao wenyewe na ndio maana wanazama katika ukafiri, upotevu, ujinga, kufuru na madhambi. Allaah amewaacha juu ya nafsi zao wenyewe. Hakuwatunuku kwa fadhila Zao. Anampa amtakaye na anamnyima amtakaye, kwa kuwa Yeye ndiye Mola wa walimwengu:

لَا يُسْأَلُ عَمَّا يَفْعَلُ وَهُمْ يُسْأَلُونَ

“Haulizwi kwa yale anayoyafanya, lakini wao wataulizwa.” 21:23

Haitakiwi kusemwa ni kwa nini amempa fulani na ni kwa nini amemwongoza fulani. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anamwongoza amtakaye na anampoteza amtakaye. Ameumba Pepo na watu wake na ameumba Moto na watu wake. Allaah atavijaza viwili hivyo:

“Pepo na Moto vitajadiliana mbele ya Mola wao. Pepo itasema: “Ee Mola! Ni kwa nini watu wadhaifu na masikini tu ndio wanaingia ndani yake?” Moto utasema: “Nimewapata wale wenye wajeuri.” Allaah (Ta´ala) atasema kuiambia Pepo: “Wewe ni huruma Wangu.” Atauambia Moto: “Wewe ni adhabu Yangu namuadhibu yule ninayemtaka.” al-Bukhaariy (7449) na Muslim (2846).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qurrat-ul-´Aynayn bi Tawdhwiyh Ma´aaniy ´Aqiydat-ir-Raaziyayn, uk. 32-33
  • Imechapishwa: 15/10/2016