Allaah (Jalla wa ´Alaa) ndiye Mkwasi, Mwenye kustahiki kuhimidiwa. Viumbe wote ni wenye kumuhitajia Allaah. Hakuna yeyote katika wao awezaye kujitosheleza kutokana na Allaah. Amesema (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا النَّاسُ أَنتُمُ الْفُقَرَاءُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَاللَّـهُ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ

“Enyi watu!  Nyinyi wote ni mafakiri kwa Allaah na Allaah ndiye Mkwasi,  Mwenye kustahiki kuhimidiwa.”[1]

Hakuna yeyote awezaye kujitosheleza kutokana na Allaah, hata kama atakuwa na ufalme wa dunia nzima. Wafalme ni wenye kumuhitaji Allaah. Matajiri wanamuhitaji Allaah.  Hakuna yeyote anayejitosheleza na Allaah, si Malaika waliokurubishwa au viumbe wengine. Atakayedai kuwa anajitosheleza kutokana na Allaah, basi anakufuru na ametoka nje ya dini. Ni wajibu kwa mja kumuonyesha Allaah unyonge wake na asijione kutokana na zile nguvu, uzima na utajiri. Kwa sababu mambo yote yako mikononi mwa Allaah (´Azza wa Jall). Haiwezekani kujitosheleza kutokana na Allaah (´Azza wa Jall).

[1]35:15

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 223
  • Imechapishwa: 20/04/2025