20. Vipi kumuosha Muhrim akifa katika hali ya Ihraam yake?

Swali 20: Vipi kumuosha Muhrim akifa katika hali ya Ihraam yake[1]?

Jibu: Muhrim akifa anaoshwa lakini hatiwi manukato, hafunikwi kichwa uso wala kichwa chake. Anavikwa sanda ndani ya Ihraam yake na wala havishwi kanzu, kilemba na mfano wa hivo. Kwa sababu atafufuliwa siku ya Qiyaamah hali ya kuwa ni mwenye kuleta Talbiyah. Hivo ndivo zilivyosihi Hadiyth kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Halipiwi yale matendo yake ya hajj yaliyobakia. Ni mamoja amekufa kabla ya ´Arafah au baada yake. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuamrisha jambo hilo.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/120).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 21-22
  • Imechapishwa: 15/12/2021