Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa kweli isipokuwa Allaah ina nguzo zake ambazo ni kukanusha na kuthibitisha.
1- Nguzo ya kwanza: Kuthibitisha. Sentesi “Hapana mungu wa kweli” inabatilisha ushirika kwa aina zake zote na wakati huohuo inawajibisha kukufuru vile vyote vinavyoabudiwa badala ya Allaah.
2- Nguzo ya pili: “Isipokuwa Allaah” inathibitisha kwamba hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allaah na inawajibisha kulitendea kazi. Maana ya nguzo mbili hizi imekuja katika Aayah nyingi kama mfano wa maneno Yake (Ta´ala):
فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ فَقَدِ اسْتَمْسَكَ بِالْعُرْوَةِ الْوُثْقَىٰ
“Basi atakayemkanusha Twaaghuut na akamuamini Allaah, hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika.”[1]
Maneno Yake:
فَمَن يَكْفُرْ بِالطَّاغُوتِ ٰ
“Basi atakayemkanusha Twaaghuut… “
ndio maana ya nguzo ya kwanza ambayo ni “hapana mungu wa kweli isipokuwa Allaah”. Maneno Yake:
وَيُؤْمِن بِاللَّـهِ
“… na akamuamini Allaah.”
ndio maana ya nguzo ya pili ambayo ni “isipokuwa Allaah”.
Kadhalika maneno Yake kuhusu Ibraahiym (´alayhis-Salaam):
إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُ سَيَهْدِينِ إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي
“Hakika mimi ni mwenye kujiweka mbali kabisa na yale mnayoyaabud. Isipokuwa Ambaye ameniumba, basi hakika Yeye ataniongoza. Isipokuwa ambaye ameniumba.. ”[2]
Maneno Yake:
إِنَّنِي بَرَاءٌ
“Hakika mimi ni mwenye kujiweka mbali kabisa… “
ndio maana ya ukanushaji katika nguzo ya kwanza. Maneno Yake:
إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي
“Isipokuwa ambaye ameniumba.. ”[3]
ndio maana ya uthibitishaji katika nguzo ya pili.
[1] 02:256
[2] 43:26-27
[3] 43:26-27
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 46-47
- Imechapishwa: 10/02/2020

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 46-47
Imechapishwa: 10/02/2020
https://firqatunnajia.com/20-sura-ya-pili-maana-ya-nashuhudia-ya-kwamba-hapana-mungu-wa-kweli-isipokuwa-allaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)