Gundi inayofanya maji kutofika kwenye ngozi wakati wa wudhuu´

Swali: Baadhi ya vidole vyangu vimepatwa na gundi yenye nguvu kabisa na inakuwa vigumu kuiondosha. Gundi hii inazuia maji kufika kwenye ngozi wakati wa kutawadha. Wakati najaribu kuiondosha nahisi madhara juu ya hilo. Nifanye nini?

Jibu: Mosi: Kabla ya kutumia gundi hii vaa mikononi mwako vifuniko vya mikono vya aina ya plastiki. Midhali unajua kuwa utagusa gundi hii basi vaa vifuniko vya mikono aina ya plastiki na vitazuia kufikiwa na kitu katika gundi hii.

Pili: Tukikadiria kuwa hukufanya hivo, je, gundi haiondoki kwa kitu chochote au kuna vitu vinavyoweza kuiondosha? Petroli au mafuta ya taa. Lakini kuna baadhi ya watu wamenambia kwamba zipo gundi ambazo haziondoki si kwa petroli wala gesi. Kusema iondoke basi sehemu ya ngozi ni lazima iondoke pia. Mfano wa gundi kama hii si lazima kuiondosha. Inatosha kupitisha maji juu yake na ukiweza kusugua wakati wa kupitisha maji ndio bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (67) http://binothaimeen.net/content/1514
  • Imechapishwa: 10/02/2020