20. Sababu ya kumi na sita ya talaka ambayo ni mwanamke kutojali na kupuuza

16 – Mwanamke asiyejali

Mke pia anayeitwa ´asiyejali` ni yule asiyemtilia umuhimu wowote mume wake wala nyumba yake. Aidha hajaribu kuitikia mahitaji yake wala matakwa yake kukiwemo matangamano ya kuishi kwa uzuri au kuyatilia umuhimu mambo ya nyumbani. Mwanamke kutoitilia umuhimu nyumba yake, watoto na mume wake ni msukumo mkubwa unaopelekea talaka. Mume katika hali hiyo atahisi kuwa mke wake hampendi au hamtilii umuhimu. Hilo linaweza kupelekea na yeye mwanaume kuwa na ususuwavu kwa mwanamke huyo. Matokeo yake mume naye asimtilie umuhimu na asimuonee huruma. Hapo ndipo huanza matatizo, kufarikiana, kuhisi ugeni na kutokuwa na mafungamano kati yao.

Ni lazima kutilia umuhimu nyumba kufanywa vizuri na pia kupatiliza kuufanya uzuri mwili na mavazi. Mwanamke kutilia umuhimu kujipura na kujipamba ni jambo zuri. Yote haya yanatakiwa na ni mambo mazuri na hufanya mume akampenda. Ni mambo yanayotakikana kwa mke ili mapungufu hayo isiwe ndio mwanya wa kumfanya akawaangalia wanawake wengine au kumuoa mwanamke mwingine.

Tunamwambia mwanamke ´ee kijakazi wa Allaah, kio chako ni mume wako. Kuwa mbele yake na ule uzuri ambao anaupenda! Kuwa mbele yake ni mwanamke mwema! Kuwa mbele yake ni mwanamke mwenye muonekano mzuri na maridadi katika mavazi yako na nyumba yako!

  • Muhusika: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Twalaaq – asbaabuhu wa ´ilaajuh, uk. 34-35
  • Imechapishwa: 16/04/2024