Amehifadhi Qur-aan zaidi lakini mtenda madhambi

Swali: Ni nani anayetangulizwa mbele kati ya aliyehifadhi pakubwa au mwenye uelewa zaidi wanapokutana?

Jibu: Anayesoma bora zaidi na mwenye kisomo kingi zaidi. Wanapolingana katika uzuri basi ambaye ana kisomo kingi zaidi. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya ´Umar bin Salamah:

“Akuongozeni yule mwenye Qur-aan zaidi kati yenu.”

Swali: Inawezekana akawa amehifadhi Qur-aan sehemu kubwa lakini hata hivyo ni mwenye kunyoa ndevu zake na mwenye kuvaa nguo inayovuka kongo mbili za miguu.

Jibu: Atatangulizwa mbele yule mwadilifu na asitangulizwe mtenda madhambi mazito.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23737/من-يقدم-للامامة-اذا-اجتمع-الاحفظ-والافقه
  • Imechapishwa: 15/04/2024