Imamu pekee anayefaa kuwaswalisha watu kwa kuketi chini

Swali: Kuna mtu alikosa swalah ambapo akaingia msikitini na kukuta bwana mmoja anaswali kwa kuketi chini. Je, aswali pamoja naye?

Jibu: Hapana, hili linamuhusu yule imamu mteule peke yake. Vinginevyo aliyeketi chini hakuswaliwi nyuma yake ikiwa sio imamu mteule. Haifai akawaswalisha watu. Jambo hilo ni maalum kwa imamu rasmi anayeswali kwa kuketi chini.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23730/حكم-الصلاة-خلف-المقعد
  • Imechapishwa: 15/04/2024