20. Ni kina nani Mtume alianza kuwalingania wakati alipodhihirisha ulingano?

Swali 20: Ni kina nani alianza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwalingania wakati alipodhihirisha ulingano?

Jibu: Wakati Allaah (Ta´ala) alipomteremshia:

وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ

“Na onya jamaa zako wa karibu.”[1]

alipanda (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mlima wa Abu Qubays na akaita kwa sauti ya juu:

“Enyi Quraysh! Enyi wana wa ´Abdu Manaaf! Enyi wana wa Haashim! Zinunueni nafsi zenu! Ziokoeni nafsi zenu kutokana na Moto! Hakika sintokufaeni mbele ya Allaah na chochote. Ee ´Abbaas bin ´Abdil-Muttwalib! Sitokufaa mbele ya Allaah na chochote! Ee Swafiyyah, shangazi yake Mtume wa Mtume wa Allaah! Sitokufaa mbele ya Allaah na chochote. Ee Faatwimah, binti yake Muhammad! Niombe chochote katika mali yangu utakacho. Sitokufaa mbele ya Allaah na chochote.”[2]

[1] 26:214

[2] al-Bukhaariy (4771) na Muslim (204).

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 96
  • Imechapishwa: 16/09/2023