20. Ni ipi hukumu ya mambo yanayofanywa na baadhi katika masherehe ya watu kupiga makofi na miluzi?

Swali 20: Ni ipi hukumu ya mambo yanayofanywa na baadhi katika masherehe ya watu kupiga makofi na miluzi?

Jibu: Hukumu ya hayo ni kwamba yametoka kwa wasiokuwa waislamu. Kwa ajili hiyo haitakiwi kwa waislamu kuyafanya. Badala yake anatakiwa kusema “Allaahu Akbar” au “Subhaan Allaah” pindi jambo linapomfurahisha. Hata hivyo haya hayatakiwi kufanywa kwa pamoja, kama wanavofanya baadhi ya watu, bali mmojammoja. Kuhusu kusema “Allaahu Akbar” au “Subhaan Allaah” kwa njia ya pamoja wakati kunapotea kitu cha kufurahisha, ni jambo halina msingi wowote kutokana na ninavyojua.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah Muhimmah, uk. 28
  • Imechapishwa: 01/03/2023