19. Ni ipi hukumu ya kufanya kazi na kushirikiana na benki zenye ribaa?

Swali 19: Ni ipi hukumu ya kufanya kazi na kushirikiana na benki zenye ribaa?

 Jibu: Kufanya kazi ni haramu. Kwa sababu maana yake ima ni kusaidiana juu ya ribaa – jambo ambalo linaingia ndani ya laana ya mlaanaji Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amemlaani mwenye kula ribaa, mwenye kuitoa, katibu wake na mwenye kuishuhudia na akasema kuwa wote wana hukumu moja – au ni kuridhia na kukubaliana na kitendo hichi. Haijuzu kuajiriwa katika mabenki yanayofanya kazi na ribaa. Hata hivyo hapana vibaya kuhifadhi pesa kutokana na haja ikiwa hatukupata njia nyingine ya kuzihifadhi. Katika hali hii hapana vibaya, kwa sharti mtu asichukue ribaa kutoka humo. Hata hivyo itakuwa haramu endapo mtu atachukua ribaa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah Muhimmah, uk. 28
  • Imechapishwa: 01/03/2023