18. Ni ipi hukumu ya kufanya mazoezi kwa kaptula na ni ipi hukumu ya kuwatazama wanaofanya hivo?

Swali 18: Ni ipi hukumu ya kufanya mazoezi kwa kaptula na ni ipi hukumu ya kuwatazama wanaofanya hivo?

Jibu: Kufanya mazoezi ni jambo linafaa ikiwa hayamshugulishi mtu na jambo la wajibu. Vinginevyo itakuwa haramu. Ikiwa mtu hana kazi nyingine isipokuwa hii kwa njia ya kwamba yanamchukua muda wake mwingi, inazingatiwa ni kupoteza wakati na dogo liwezalo kusemwa katika hali hii ni kuwa inachukiza.

Lakini ikiwa wafanyaji mazoezi wamevaa kaptula kwa njia ya kwamba paja, sehemu yake kubwa inaonekana, basi haitojuzu. Maoni sahihi ni kwamba ni lazima kufunika mapaja na haijuzu kuwatazama wachezaji wakiwa katika hali kama hii.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As-ilah Muhimmah, uk. 26
  • Imechapishwa: 01/03/2023