Nilisoma namna ambavo Abu ´Abdillaah bin Abiy Hafsw al-Bukhaariy, ambaye alikuwa Shaykh wa Bukhaaraa na mmoja katika maswahiba wakubwa wa Muhammad bin al-Hasan ash-Shaybaaniy, amesimulia kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Uthmaan – yaani ´Abdaan, Shaykh wa Marw – aliyesema: Nimemsikia Muhammad bin al-Hasan ash-Shaybaaniy akisema: Hammaad bin Abiy Haniyfah amesema:
”Tuliwaambia watu hawa: ”Zingatieni juu ya maneno Yake Allaah (´Azza wa Jall):
وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا
“… na atakapokuja Mola wako na Malaika safu kwa safu.”[1]
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن يَأْتِيَهُمُ اللَّـهُ
”Je, wanangojea nini isipokuwa Allaah awajie.”[2]
Je, Mola wetu atakuja kama Alivosema? Je, Malaika watakuja wakiwa safu kwa safu?” Wakasema: ”Malaika watakuja wakiwa safu kwa safu. Kuhusu Mola wetu (Ta´ala), hatujui anakusudia nini kwa ujio Wake.” Tukasema: ”Sisi hatujakulazimisheni mjue atakuja namna gani; tulichokulazimisheni ni nyinyi kuamini kuja Kwake. Mnamuonaje yule ambaye anapinga kuwa Malaika watakuja wakiwa safu kwa safu?” Wakasema: ”Kafiri mwenye kukadhibisha.” Ndipo tukasema: ”Basi vivyo hivyo ambaye anapinga kuwa Mola (Subhaanah) atakuja ni kafiri mwenye kukadhibisha.”
Nilisoma namna Abu ´Abdillaah bin Abiy Hafsw al-Bukhaariy aliandika kwenye kitabu chake kwamba Ibraahiym bin al-Ash´ath ameeleza kuwa amemsikia al-Fudhwayl bin ´Iyaadhw akisema:
”Jahmiy akikwambia kuwa yeye hamwamini Mola anayeshuka chini kutoka mahali Pake, basi wewe mwambie kuwa unamwamini Mola anayefanya Akitakacho.”
[1] 89:22
[2] 2:210
- Muhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 232-235
- Imechapishwa: 11/12/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)