al-Awzaa´iy amesema:

“Elimu ni yale waliyokuja nayo Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mengine yote yasiyokuwa hayo sio elimu.”[1]

Imaam Ahmad pia alisema mamna hiyo na akasema kuhusu wanafunzi wa Maswahabah:

“Uko na khiyari.”

Bi maana uko na khiyari ya kuandika au kuacha kuandika elimu yao. az-Zuhriy alikuwa akiandika elimu yao na Swaalih bin Kaysaan akaenda kinyume naye ambapo akajutia kuacha kuandika maneno ya wanafunzi wa Maswahabah. Khaswa hii leo ni lazima kuandika maneno ya maimamu wa Salaf wanaofatwa mpaka katika zama za ash-Shaafi´iy, Ahmad, Ishaaq na Abu ´Ubayd. Kisha mtu awe na tahadhari juu ya yale yaliyozuka baada yao, kwa sababu kumezuka baada yao mambo mengi mepya. Miongoni mwa mambo hayo mepya ni watu kutoka katika Dhwaahiriyyah na mfano wao wanaojinasibisha na Sunnah na Hadiyth, lakini ukweli wa mambo ni wenye kupinda kutokamana nayo vibaya sana kwa sababu ya kwenda kwao kinyume na ufahamu wa maimamu na kuendea ufahamu wake mwenyewe au akaonelea yale ambayo hayakuonelewa na maimamu kabla yake.

[1]Jaami´ Bayaan-il-´Ilm wa Fadhwlih (2/29).

  • Muhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Fadhwl ´Ilm-is-Salaf ´alaa ´Ilm-il-Khalaf, uk. 68-69
  • Imechapishwa: 22/09/2021