Mtu mwenye akili sahihi na maumbile yaliyosalimika akiyazingatia mambo haya makubwa atajua kuwa Qiyaamah ni haki na atatambua kuwa yale yanayodaiwa na wakanamungu, wakomunisti, waabudia mizimu na wengineo ambao wanakanusha Aakhirah na miili kuumbwa upya ni batili iliokuwa kubwa na itambainikia kuwa madai yao ni ya batili na maneno yao ni ya uongo.

Vivyo hivyo watu wa makundi mbalimbali, linganizi zinazopotosha na fikira za kuangamiza wote wako katika njia hii pale anapozingatia yule ambaye ana akili sahihi, utambuzi wenye kutekelezwa na maumbile yaliyosalimika atatambua upotofu wao na atatambua kuwa dalili ya uwongo wao kutoka ndani ya Qur-aan na Sunnah na kutoka ndani ya vitabu sahihi.

Hakika Yeye (Subhaanah) ameumba vitu vyenye kuonekana na akasimamisha dalili juu ya haki kutoka ndani ya Kitabu Chake na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwa yale aliyoyaweka kwenye akili katika ufahamu na kuyaelewa mambo na kwa yale aliyoyaumba katika ulimwengu huu katika viumbe. Vyote hivo vinatoa ushuhuda kwa hekima na kwamba Yeye ndiye Muumba, Mwenye hekima, Mwenye kuruzuku, Mkarimu, Muweza juu ya kila jambo na Mwenye kustahiki kuabudiwa Mwenyewe asiyekuwa na mshirika.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamiyyat-ul-´Ilm https://binbaz.org.sa/discussions/33/اهمية-العلم-في-محاربة-الافكار-الهدامة
  • Imechapishwa: 18/05/2022