20. Inafaa kwa mwanamke kufuta kichwa chake kilichopakwa hina?

Swali 20: Je, inafaa kwa mwanamke kupangusa kichwa chake ikiwa amekipaka hina na mfano wake?

Jibu: Inafaa kwa mwanamke kufuta kichwa chake kama amekipaka hina. Hakuna haja kwa yeye kuondoa hina hii. Imethibiti kwamba kichwa cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kilikuwa kimepakwa hina alipokuwa katika Ihraam. Hina iliopakwa katika kichwa ni sehemu ya kichwa. Hili linafahamisha kwamba kuna wepesi katika kusafisha kichwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Buhuuth wa Fataawaa fiyl-Mas´h ´alaal-Khuffayn, katika Majmuu´-ul-Fataawaa (11/171)
  • Imechapishwa: 06/05/2021