20. Haya ndio malengo ya wenye kuwatetea Ahl-ul-Bid´ah

Kuhusu wale wanaosema kuwa suala la kusema kuwa Qur-aan imeumbwa hayahitajii kutiliwa umuhimu mkubwa hivo na kwamba ni katika mambo yasiyokuwa na maana yoyote. Haya yanasemwa na baadhi ya waandishi wa leo wapotofu na wenye kujifanya kuwa ni wanazuoni. Haya ni maneno batili na kuchukulia wepesi suala la khatari mno. Haifai kulichukulia sahali. Haya si mambo yasiyokuwa na maana. Huku ni kuwadharau wanazuoni waliosimama kidete kuiraddi na wakaadhibiwa walioadhibiwa, kama Imaam Ahmad, na wakauawa waliouawa katika wao kwa sababu ya kuiraddi. Halafu baada ya haya yote anakuja mtu na kusema kuwa ni mambo madogo tu na hayahitaji yote haya. Mtu huyu ima ni mjinga asiyetambua kitu au anajifanya kuwa ni mjinga na ni mpotevu. Lengo lake anataka wasiraddiwe Jahmiyyah, Mu´tazilah na Ashaa´irah.

Kuna wengine wanaosema kuwa watu wako huru na kwamba watu wasikatane kwa sababu kila mmoja ana uhuru wa kuzungumza. Hii ina maana kwamba batili isiraddiwe na haki isibainishwe. Kila mmoja azungumze anachokitaka. Kwa kufanya hivi dunia nzima itajaa vurugu. Ni wajibu kuzinduka na propaganda kama hizi na shari hizi zinazoenezwa dhidi ya waislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 70-71
  • Imechapishwa: 31/12/2023