19. Qur-aan sio maneno ya Allaah – njama za kiyahudi

Ni njama za kiyahudi. Kwa kuwa msingi wa madhehebu ya Jahmiyyah yamechukuliwa kutoka kwa mayahudi. Hivyo ndivyo alivyosema Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) katika kitabu chake “al-Hamawiyyah”[1]. Amesema kuwa yamechukuliwa kutoka kwa mayahudi. Hili sio jambo la ajabu au geni kwa mayahudi Allaah awalaani. Wameyapotosha maneno ya Allaah, wakayabadili na kuyageuza. Hizi ni kampeni za mayahudi ili waibatilishe Qur-aan ilio kwenye mikono ya waislamu. Hii ni ´Aqiydah chafu. Kwa ajili hii ndio maana maimamu wakasimama kidete kuiraddi na kuibatilisha na kubainisha kuwa ni kampeni zilizopenyezwa.

[1] Tazama “al-Hamawiyyah al-Kubraa”, uk. 232-235

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 70
  • Imechapishwa: 31/12/2023