Mapote yote haya, mbali na Jahmiyyah, nadharia zote za mapote haya zinakataliwa na mlango “Kutoka katika imani kwa sababu ya madhambi”. Kuhusiana na Jahmiyyah, wanaraddiwa na watu wote wa dini. Qur-aan pia inawakadhibisha pale iliposema:

يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمْ

“Wanatambua kama wanavyowatambua watoto wao.”[1]

na:

وَجَحَدُوا بِهَا وَاسْتَيْقَنَتْهَا أَنفُسُهُمْ ظُلْمًا وَعُلُوًّا

“Wakazipinga kwa dhuluma na majivuno na hali kuwa nafsi zao zimeziyakinisha. ”[2]

Allaah amekhabarisha juu ya kukufuru kwao kwa sababu wamekanusha kwa ndimi zao licha ya kwamba wanatambua kwa nyoyo zao. Kisha Allaah (´Azza wa Jall) akaeleza ya kwamba Ibliys alikuwa ni katika makafiri ingawa anamtambua Allaah kwa moyo na ulimi wake. Zipo dalili nyingi ambazo kutarefuka kuzitaja hapa na hivi sasa. Zote zinarudisha na kuisambaratisha ´Aqiydah yao kwa njia ngumu na ya ukali kabisa.

Mwisho wa kitabu

Kijitabu kimeandikwa kwa hati ya mkono katika Shawwaal 488 kutokana na nakala aliyoipata Shaykh al-´Afiyf Abu Muhammad ´Uthmaan bin Abiy Naswr Misri na ambayo baadaye ikalinganishwa nayo. Himdi zote njema anastahiki Allaah pekee!

[1] 2:146

[2] 27:14

  • Mhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 102-103
  • Imechapishwa: 04/07/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naawswir-ud-Diyn al-Albaaniy