370 – ´Ubaadah bin as-Swaamit (Rahdiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

خمسُ صلواتٍ كتبهُنَّ اللهُ على العبادِ، فمَن جاء بهنَّ، ولم يُضَيِّع مِنهنَّ شيئاً استخفافاً بحقّهنَّ؛ كان له عندَ اللهِ عهدٌ أنْ يُدخلَه الجنّةَ، ومَن لمْ يأتِ بهنَّ، فليس له عندَ اللهِ عهد؛ إنْ شاءَ عذَّبه، وإنْ شاء أدخله الجنّةَ

“Swalah tano Allaah amewafaradhishia waja. Yule mwenye kuzitekeleza na asipoteza kitu katika hizo kwa ajili ya kuzidharau, basi atakuwa na ahadi kwa Allaah ya kumwingiza Peponi. Na yule asiyezitekeleza, basi hana ahadi yoyote kwa Allaah; akitaka atamuadhibu na akitaka atamwingiza Peponi.”[1]

Ameipokea Maalik, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy na Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” yake. Imekuja kwa Abu Daawuud:

خمسُ صلواتٍ افترَضَهُنَّ اللهُ، من أحسن وضوءَهنَّ بوقتهنَّ، وأتمّ رُكوعَهنَّ، وسجودَهنَّ، وخشوعَهنَّ؛ كان له على الله عهدٌ أنْ يَغفرَ له، ومَن لمْ يفعلْ؛ فليس له على اللهِ عهدٌ؛ إنْ شاءَ غَفر له، وإنْ شاءَ عذَّبه

 “Allaah amefaradhisha swalah tano. Ambaye atatia vizuri wudhuu´ wake ndani ya nyakati zake na akatimiza Rukuu´ zake, Sujuud na unyenyekevu, basi  atakuwa na ahadi kwa Allaah ya kumsamehe. Ambaye hatofanya hivo, basi hana ahadi yoyote kwa Allaah; akitaka atamsamehe na akitaka atamuadhibu.”

[1] Swahiyh kupitia zingine.

Miongoni mwa maana za Hadiyth hii ni pamoja na yale aliyosema Abu ´Abdillaah bin Battwah:

“Mtu hatoki katika Uislamu isipokuwa kwa kumshirikisha Allaah au kurudisha faradhi miongoni mwa faradhi za Allaah (´Azza wa Jall) kwa kuikanusha. Akiacha kwa uzembe au uvivu, basi anaingia ndani ya utashi wa Allaah; akitaka atamuadhibu na akitaka atamsamehe.” (ash-Sharh wal-Ibaanah (73))

Haipingani na Hadiyth zinazokuja huko mbele, kwa sababu zinahusiana na yule mwenye kukaidi na mwenye kufanya kiburi, kama nitakavyotaja huko.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/271-272)
  • Imechapishwa: 28/08/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy