Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:
11 – Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kuleni daku. Kwani hakika katika daku kuna baraka.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Hadiyth hii ni dalili kwamba mwenye kufunga ameamrishwa kula daku. Daku inayo kheri nyingi na baraka kubwa, za kidini na za kidunia. Kutaja kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baraka ni kwa lengo la kuhimiza kula daku na kuwatia watu shauku juu yake. Daku ni kile chakula kinacholiwa mwishoni mwa usiku.
Amri iliyopo katika Hadiyth hii ni amri ya kupendekezw si ya lazima. Ibn-ul-Mundhir (Rahimahu Allaah) ameeleza maafikiano ya jambo hilo. Dalili ya hilo ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwahi kuunganisha swawm na vivyo hivyo Maswahabah wake wakafanya hivo. Kuunganisha swawm kufunga siku mbili na zaidi na mtu hafungui. Kwa msemo mwingine mfungaji anafunga mchana na usiku, kama inavyokuja mbele – Allaa akitaka.
[1] al-Bukhaariy (1923) na Muslim (1095).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/30)
- Imechapishwa: 09/02/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)