Haafidhw Ibn Hajar al-´Asqalaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:
9 – Sahl bin Sa´d (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Watu hawatoacha kuwa juu ya kheri muda wa kuwa wanaharakisha kukata swawm.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
10 – at-Tirmidhiy amempokea Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah (´Azza wa Jall) amesema: “Waja wangu ninaowapenda zaidi ni wale wanaoharakisha kukata swawm.”[2]
Hadiyth hii ni dalili ya kupendekezwa kwa kuharakisha kufuturu na kulifanya mara tu wakati wake unapowadia, nao ni pale tu jua linapozama. Huo ndio mwenendo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hivyo inapaswa kufuatwa mwongozo wake na kushikamana barabara na Sunnah zake.
Katika kuharakisha ukataji swawm kuna wepesi kwa watu na kujieka mbali na sifa ya kuvuka na kuchupa mipaka katika dini. Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – ambao ndio watu wa karne bora – walilifanyia kazi jambo hili. al-Bukhaariy amesema:
“Abu Sa´iyd alikata swawm mara tu jua lilipozama.”[3]
´Amr bin Maymuun al-Awdiy (Rahimahu Allaah) amesema:
“Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa ni watu wenye haraka zaidi katika kukata swawm na waliochelewesha zaidi daku.”[4]
Kwa hiyo muislamu anapaswa kujitahidi kufanyia kazi Sunnah hii ya kuharakisha kukata swawm. Miongoni mwa njia za kusaidia hilo ni kutenga muda wa mwisho wa mchana kwa kusoma ajili ya Qur-aan, kumtaja Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na kufanya du´aa na wala asitoke nyumbani kwa jambo lisilo la lazima ili asijipotezee kheri hii. Muadhini anaweza kuadhini wakati yeye akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake na hivyo akafika akiwa amechoka, amepoteza wakati wa kuomba du´aa na kukosa kuharakisha kukata swawm – na msaada ni wenye kuombwa kwa Allaah.
[1] al-Bukhaariy (1957) na Muslim (1098).
[2] at-Tirmidhiy (700). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (700).
[3] “Fath-ul-Baariy” (04/196).
[4] ´Abd-ur-Razzaq (04/226). Haafidhw Ibn Hajar amesema:
”Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh.” (Fath al-Bari (4/199)).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/26)
- Imechapishwa: 09/02/2025

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Minhat-ul-´Allaam fiy Sharh Buluugh-il-Maraam (05/26)
Imechapishwa: 09/02/2025
https://firqatunnajia.com/19-hadiyth-watu-hawatoacha-kuwa-juu-ya-kheri/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)