Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

Kwa ajili hii jopo la Salaf, akiwemo ath-Thawriy (Rahimahumu Allaah), wamesema:

“Bid´ah ni yenye kupendeza zaidi kwa Ibliys kuliko maasi.”

Kwa sababu maasi mtu hutubia kwayo. Bid´ah mtu hatubii kwayo. Hii ndio maana ya yale yaliyopokelewa na jopo katika wao kwamba:

“Hakika Allaah amezuia tawbah ya kila mzushi.”

Maana yake ni kwamba hatubii kwayo kwa sababu anaona kuwa yuko juu ya uongofu. Lakini endapo atatubu basi Allaah atamsamehe kama alivyomsamehe kafiri. Ambaye amesema kuwa tawbah yake haikubaliwi kabisa amekosea kosa kubwa. Ambaye amesema:

“Allaah hampi idhini mzushi katika tawbah.”

Maana yake ni kwamba hasamehewi muda wa kuwa ni mzushi na anaona anachokifanya ni kizuri. Lakini Allaah akimjaalia kumuonyesha kuwa ni kibaya, basi anamsamehe kama ambavo anamjaalia kafiri kuona kuwa yuko kwenye upotevu. Vinginevyo wako wengi ambao walikuwa juu ya Bid´ah baadaye wamekuja kubainikiwa na upotevu wao na hivyo Allaah akawasemehe. Watu hao hawadhibitiwi[1]. Allaah ndiye mjuzi zaidi na swalah na salamu zimwendee Mtume wetu Muhammad[2].

MAELEZO

Hii ndio haki. Hakika Allaah amezuia tawbah ya mzushi kwa sababu anaona kuwa ni nzuri na anaona kuwa ni mwenye kupatia. Ndio maana mara nyingi anakufa juu yake na hatubii kwayo. Kwani anaona kuwa ni mwenye kupatia. Hali hiyo ni tofauti na mtenda madhambi ambaye anatambua kuwa yuko katika madhambi, kwamba ni haramu na kwamba ni mwenye kukosea. Mtu kama huyu anaweza kutubia ambapo Allaah akamsamehe. Lakini mzushi yuko khatarini. Kwa sababu anaifanya kuwa nzuri na anafuata matamanio yake. Kwa ajili hi mzushi yuko khatarini kuzuiliwa tawbah yake kwa sababu ya kule kuionelea kuwa ni nzuri na kufikiria kuwa yuko juu ya uongofu na imani. Vinginevyo Allaah akimwongoza na akatubu, basi Allaah anasamehe madhambi yote muda wa kuwa mja atatubia kwayo. Mpaka shirki ambayo ndio dhambi kubwa kuliko Bid´ah, lakini mtu akitubia kwayo basi Allaah humsamehe. Makafiri katika Quraysh na wengineo walipotubu Allaah akawasamehe. Vivyo hivyo wachawi wa Fir´awn wakati walipotubu Allaah akawasamehe. Kadhalika mzushi Allaah akimjaalia akatubu basi Allaah humsamehe. Ni kwa lengo la matishio kama mfano wa Hadiyth Swahiyh:

”Yule mwenye kuzusha uzushi au akamsaidia mzushi, basi juu yake iko laana ya Allaah, Malaika na watu wote. Allaah hatokubali kutoka kwake [siku ya Qiyaamah] tawbah wala fidia.”[3]

Hii ni kwa njia ya matishio. Vinginevyo yule mwenye kutubu Allaah humsamehe.

[1] Mamuu´-ul-Fataawaa (11/684).

[2] Haya amesomewa Shaykh Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) jioni mwa siku ya jumapili sawa na tarehe 9 Rabiy´ al-Awwaal 1418.

[3] al-Bukhaariy (1870) na Muslim (1370).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fadhwl-il-Islaam, uk. 35-36
  • Imechapishwa: 04/11/2020