19. Miongoni mwa khatari na majanga ya Bid´ah

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Yamepokelewa katika Hadiyth ya Anas bin Maalik pamoja na al-Hasan al-Baswriy kwa mfuatano wa wasimulizi uliokatika kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ibn Wadhdhwaah ameeleza kuwa Ayyuub amesema:

“Kuna mtu katika sisi aliyekuwa na ´Aqiydah mbovu na baadae akaiacha. Nikamwendea Muhammad bin Siriyn na kumwambia: “Je, unajua kuwa fulani ameacha ´Aqiydah yake?” Akasema: “Tazama amegeuka kuwa nini. Sehemu ya mwisho ya Hadiyth pigo zaidi kwao kuliko sehemu yake ya mwanzo:

“Wanatoka nje ya Uislamu kisha hawarudi tena.”[1]

Ahmad bin Hanbal aliulizwa maana yake akajibu:

“Hawawafikishwi kutubu.”

MAELEZO

Miongoni mwa khatari na majanga ya Bid´ah ni kwamba mwenye nayo hawafikishwi kutubia. Kwa sababu anajiona kuwa ni mwenye kupatia na hivyo anaendelea juu ya batili. Hili ni moja ya majanga na khatari zake. Kwa hivyo ni lazima kutahadhari kutokamana na Bid´ah. Ni yenye shari kubwa. Ndio maana amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuzusha katika amri yetu hii yasiyokuwemo yatarudishwa.”

Amesema:

”Kila Bid´ah ni upotevu.”

[1] Muslim (1067).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fadhwl-il-Islaam, uk. 27-28
  • Imechapishwa: 04/11/2020