Hedhi ni damu ya kimaumbile inayomtoka mwanamke bila ya sababu na inatoka katika nyakati maalum. Damu hii ni ya kimaumbile ambayo haitokamani na maradhi, donda, kuanguka au kuzaa. Kwa vile ni damu ya kimaumbile, inatokamana na hali ya mwanamke, mazingira yake na hali ya hewa. Kwa sababu hiyo hedhi ya wanawake inatofautiana wazi.

Hekima ni kwa sababu pale ilipokuwa mtoto ndani ya tumbo la mama yake hawezi kula chakula cha kawaida au kulishwa nacho na mama, ndipo Allaah (Ta´ala) akapanga msuguano wa kidamu ambao mtoto anakula kupitia msuguano huo bila ya kuwa na haja ya kula wala kutafuna. Chakula hicho kinaingia katika kiwiliwili chake kupitia njia ya kitovu; damu inapita kwenye mishipa ya mtoto na ikawa ndio chakula chake. Amekuwa na baraka Allaah, mbora wa wenye kuumba! Hii ndio hekima ya hedhi hii. Kwa ajili hiyo pale mwanamke anaposhika ujauzito hedhi yake inakatika. Ni nadra mwanamke mjamzito akapata hedhi. Kadhalika mwanamke mwenye kunyonyesha hedhi yake husita na khaswa katika kile kipindi cha mwanzo cha kunyonyesha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Dimaa’ at-Twabiy´iyyah lin-Nisaa’ http://www.ibnothaimeen.com/all/books/article_16961.shtml
  • Imechapishwa: 29/10/2016