2. Jina la mtoto linatakiwa kuwa la kiarabu

Moja katika sifa muhimu ya jina lisifanane na majina ya maadui wa Allaah. Baadhi ya ndugu zetu wa dini moja wanapigania ni nani atampa mtoto majina kama hayo. Hii ni natija ya utandawazi, vyombo vya khabari haribifu, ughafilikaji wa baadhi ya watu, ujinga wa wengine na kukosekana kwa sifa nzuri. Utakasifu ni Wako Allaah! Ni wangapi wametumbikia katika mtego huu.

Hali zao zinasikitisha. Vinginevyo itakuwa vipi wakati unamuona ana chimbuko la Kiislamu utafikiri ni kama mkufu wa dhahabu kisha unamuona jinsi anavyotupwa huku na huku katika matamanio na kumpa mtoto wake jina la kimagharibi? Anampa jina la wale walioghadhibikiwa katika mayahudi, manaswara, wakomunisti na nyumati zingine za makafiri.

Ni wajibu kwa waislamu wote kwa jumla na khaswa wailsamu katika kisiwa cha Kiarabu kuwapa watoto wao majina yasiyoenda kinyume na Shari´ah kwa njia yoyote ile na yawe ya kiarabu. Wakati mtu anakuja katika mji wao au wakati wao wanasafiri kwenda katika mji basi wengine wasisikie ila jina ´Abdullaah, ´Abdur-Rahmaan, Ahmad, ´Aaishah, Faatwimah na majina mengine yote ya Kishari´ah ambayo ni mengi kuyataja na ambayo yanapatikana katika vitabu vya wasifu na vya kihistoria.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 03-04
  • Imechapishwa: 18/03/2017