Himdi zote ni za Allaah. Tunamhimidi Yeye na kumuomba msaada na msamaha. Tunajikinga Kwake kutokana na shari ya nafsi zetu na matendo yetu maovu. Yule mwenye kuongozwa na Allaah, basi hakuna awezae kumpoteza, na yule mwenye kupotezwa na Allaah, basi hakuna awezae kumwongoza. Ninashuhudia ya kwamba hapana mola wa haki isipokuwa Allaah na ninashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake.

Amma ba´d:

Hakika jina linaonesha ni nani na ni nini yule mpewa jina na vipi uhusiano unatakiwa kuwa na mtu huyo. Ni mapambo kwa mtoto na dalili anayoitiwa kwayo duniani na Aakhirah. Linaonesha dini ya mtoto na kuonesha kuwa ni katika wafuasi wake. Tazama wale wenye kuingia katika dini ya Allaah Uislamu jinsi wanavobadilisha majina yao asli kwenda katika majina ya Kiislamu, kwa sababu jina ni alama.

Isitoshe jina ni alama yenye kufichukua mwelekeo wa baba na kigezo chenye kuweka wazi msimamo wake wa dini. Jina lina maana na mwelekeo wake kwa watu. Wanalitazama jina kama mavazi; likiwa lifupi linakuwa libaya na likiwa lirefu linakuwa libaya.

Ndio maana imeandikwa katika Shari´ah na katika lugha ya kiarabu ya kuwa utoaji jina ni haki ya baba ili yule mtoto mchanga anayezaliwa asije kupewa jina lenye kumfanya akawa mbaya.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 03
  • Imechapishwa: 18/03/2017