195. Kila kinachotokea, kinatokea kwa matakwa ya Allaah

Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

147 – Kila kitu kinatokea kwa matakwa ya Allaah (Ta´ala), ujuzi, mipango na makadirio Yake.

MAELEZO

Hakuna chochote kinachotokea katika ufalme Wake isipokuwa kwa utambuzi na kukadiria Kwake:

وَمَاتَشَاءُونَإِلَّاأَنيَشَاءَاللَّـهُرَبُّالْعَالَمِينَ

”Hamtotaka isipokuwa atake Allaah, Mola wa walimwengu.”[1]

Kila kitu kinachotokea katika ulimwengu amekipanga, kukikadiria na ameakiandika katika Ubao uliohifadhiwa.

[1]81:29

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 213-214
  • Imechapishwa: 15/04/2025