Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
147 – Hiyo ndio tafsiri ya hapana kutikisika wala namna isipokuwa kwa msaada wa Allaah. Hakuna yeyote awezaye kumuasi Allaah isipokuwa kwa msaada wa Allaah. Wala hakuna yeyote awezaye kumtii Allaah kwa kudumu isipokuwa kwa kuwafikishwa na Allah.
MAELEZO
Hakuna awezaye kubadilika kutoka katika hali moja kwenda katika hali nyingine isipokuwa kwa msaada wa Allaah (Jalla wa ´Alaa). Wala huna nguvu zozote isipokuwa nguvu za Allaah (´Azza wa Jall). Hapa kuna kujisalimisha na kujitenga mbali kutokana na matikisiko na nguvu. Mtu asijikweze kwa kutikisika na nguvu zake, isipokuwa anataka kurejea kwa Allaah (´Azza wa Jall) na kumuomba msaada, ili akusaidie kutoka katika maasi na kwenda katika utiifu, kukutoa katika ukafiri na kukuingiza katika Uislamu. Kila kitu kinatokana na matikiso na nguvu za Allaah. Endapo angekuegemeza katika matikiso yako mwenyewe, basi kamwe usingeliweza. Vivyo hivyo inahusiana na bidii, kuchuma na mahangaiko yako kuitafuta mali; ni kweli wewe ndiye ambaye unahangaika na kupambana, lakini kuwafikishwa na baraka ni zenye kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 213
- Imechapishwa: 15/04/2025
Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
147 – Hiyo ndio tafsiri ya hapana kutikisika wala namna isipokuwa kwa msaada wa Allaah. Hakuna yeyote awezaye kumuasi Allaah isipokuwa kwa msaada wa Allaah. Wala hakuna yeyote awezaye kumtii Allaah kwa kudumu isipokuwa kwa kuwafikishwa na Allah.
MAELEZO
Hakuna awezaye kubadilika kutoka katika hali moja kwenda katika hali nyingine isipokuwa kwa msaada wa Allaah (Jalla wa ´Alaa). Wala huna nguvu zozote isipokuwa nguvu za Allaah (´Azza wa Jall). Hapa kuna kujisalimisha na kujitenga mbali kutokana na matikisiko na nguvu. Mtu asijikweze kwa kutikisika na nguvu zake, isipokuwa anataka kurejea kwa Allaah (´Azza wa Jall) na kumuomba msaada, ili akusaidie kutoka katika maasi na kwenda katika utiifu, kukutoa katika ukafiri na kukuingiza katika Uislamu. Kila kitu kinatokana na matikiso na nguvu za Allaah. Endapo angekuegemeza katika matikiso yako mwenyewe, basi kamwe usingeliweza. Vivyo hivyo inahusiana na bidii, kuchuma na mahangaiko yako kuitafuta mali; ni kweli wewe ndiye ambaye unahangaika na kupambana, lakini kuwafikishwa na baraka ni zenye kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall).
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 213
Imechapishwa: 15/04/2025
https://firqatunnajia.com/194-usiikwaze-nafsi-yako/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)