19. Wewe si pekee uliyepatwa na msiba

Bwana mmoja aliulizwa ana watoto wangapi. Akajibu:

“Tisa.” Akaambiwa: “Sisi tunamjua mmoja tu.” Akasema: “Nilikuwa na kumi, lakini tisa wakatangulia mbele ya haki. Nimebaki na mmoja. Sijui kama mimi ni wake au yeye ni wangu.”

Imepokelewa kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan, mpwa wa al-Aswma´iy, aliyesimulia kutoka kwa ami yake, ambaye amesema:

“Alikuwa anakuja bibi mmoja mzee kutoka katika Bakr bin Kilaab. Watu wakizungumzia juu ya akili yake na uimara wake. Amenihadidthia mimi mmoja katika waliokuwa wakihudhuria kwake. Akafariki mwanawe wa kiume na alikuwa ndiye mwana pekee. Alikuwa mgonjwa kwa kipindi kirefu na akamuuguza vizuri. Alipokufa, akaketi katika uwanja wake na wakahudhuria watu wake. Akamwelekea mzee mmoja kati yao na akasema: “Ee fulani! Ni ipi haki ya ambaye aliishi akiwa mzima, akamiminiwa neema na katika maumbile kwa njia ya kwamba anaepuka kujizuia kabla ya kujiachilia, kupata adhabu yake na kufikwa na kifo ya ndani nyumba yake?” Kisha akasoma mashairi:

Yeye ni mwanangu ambaye nayasahau malipo yake kwangu

Mola ameniliwaza juu ya nafsi yake – ni Yake

Nikitaraji malipo, nitalipwa ujira

na ikiwa nitalia, basi ni kama mwanamke anayelia ambaye kulia kwake hakuna maana yoyote

Ndipo mzee yule akasema: “Tulikuwa tukisikia kuwa wanawake pekee ndio wenye kukata tamaa. Hakuna mwanamme yeyote atakayekata tamaa baada yako. Subira yako ni tukufu. Hufanani na wanawake wengine.” Akamwelekea kwa uso wake na akasema: “Hakuna jambo linalopambanua kati ya kukata tamaa na subira isipokuwa utapata namna ambavyo hali mbili hizo zinatofautiana. Subira inaonekana vizuri na mwisho wake ni wenye kusifiwa. Kuhusu kukata tamaa si vyengine isipokuwa tu dhambi; wala mtu habadilishiwi kwa kile alichopoteza. Endapo mawili hayo yangelikuwa katika maumbile ya wanamme wawili wazuri, basi subira ingelikuwa na haki zaidi ya kushinda, nzuri na tukufu zaidi inapokuja katika dini duniani na malipo Aakhirah. Inatosha kuwa Allaah (´Azza wa Jall) amemuahidi thawabu yule ambaye amemtunukia jambo hilo.”

Kulisemwa kuambiwa bedui mmoja ambaye alikufa mwanawe akasubiri:

“Ni uzuri uliyoje ulivyolichukulia jambo hilo!” Ndipo akasema: “Kumpoteza kunanidhaminisha msiba wangu baada yake.”

Baadhi waliimba mashairi yenye maana:

Hakuna nilichokuwa naogopa kama yeye kufa

Hivi sasa hakuna kingine ninachoogopa

Amesema mwingine:

Nilikuwa nakhofu kabla ya kufa kwao

Wakati walipokufa basi kamwe sikuwa tena mwenye kuogopa

Mwingine amesema:

Wacha afe anayetaka baada yako –

masaibu yako ndio niliyokuwa nachelea

Ma´n bin Aws amesema:

Tambua kuwa sijapatapo kupatwa na msiba wowote

isipokuwa umempata pia kijana fulani kabla yangu

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin ´Abdillaah bin Naaswir-id-Diyn ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bard-ul-Akbaad ´inda Faqd-il-Awlaad, uk. 93-95
  • Imechapishwa: 20/08/2023