39 – Ahmad bin ´Amr ametukhabarisha: Yuunus bin ´Abdil-A´laa ametuhadithia: Ibn Wahb ametuhadithia: Yuunus ametukhabarisha, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Humayd bin ´Abdir-Rahmaan bin Wahb, ambaye ameeleza kuwa amemsikia Abu Hurayrah amemsimulia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Aadam na Muusa walizozana mbele ya Mola wao ambapo Aadam akamshinda Muusa. Muusa alisema: ”Wewe ndiye yule ambaye Allaah amekuumba kwa mkono Wake, akakupulizia roho Yake, awafanya Malaika Wake kukusujudia na akakukaza Peponi, ambapo ukatufanya ukafanya kutokana na dhambi yako watu kuteremshwa ardhini.” Ndipo Aadam akamwambia: ”Wewe ndiye Muusa ambaye Allaah amekuteua kwa ujumbe Wake na kwa maneno Yake, akakupa Tawraat ambayo ndani yake kuna ubainifu wa kila kitu na akakukurubisha kwa ajili ya kukunong´oneza. Ni lini uliona kuwa Allaah ameandika Tawraat kabla ya kuniumba mimi?” Akasema: ”Miaka arobaini kabla.” Aadam akasema: ”Je, hukupata ndani yake:
وَعَصَىٰ آدَمُ رَبَّهُ فَغَوَىٰ
”Aadam akamuasi Mola Wake akapotoka.”[1]?
Akasema: ”Ndio.” Ndipo akasema: ”Je, unanilaumu kwa kufanya jambo ambalo Allaah aliniandikia miaka arobaini kulifanya kabla ya Yeye kuniumba?” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Aadam akamshinda Muusa.”
[1] 20:121
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 69
- Imechapishwa: 15/06/2026
- Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
39 – Ahmad bin ´Amr ametukhabarisha: Yuunus bin ´Abdil-A´laa ametuhadithia: Ibn Wahb ametuhadithia: Yuunus ametukhabarisha, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Humayd bin ´Abdir-Rahmaan bin Wahb, ambaye ameeleza kuwa amemsikia Abu Hurayrah amemsimulia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Aadam na Muusa walizozana mbele ya Mola wao ambapo Aadam akamshinda Muusa. Muusa alisema: ”Wewe ndiye yule ambaye Allaah amekuumba kwa mkono Wake, akakupulizia roho Yake, awafanya Malaika Wake kukusujudia na akakukaza Peponi, ambapo ukatufanya ukafanya kutokana na dhambi yako watu kuteremshwa ardhini.” Ndipo Aadam akamwambia: ”Wewe ndiye Muusa ambaye Allaah amekuteua kwa ujumbe Wake na kwa maneno Yake, akakupa Tawraat ambayo ndani yake kuna ubainifu wa kila kitu na akakukurubisha kwa ajili ya kukunong´oneza. Ni lini uliona kuwa Allaah ameandika Tawraat kabla ya kuniumba mimi?” Akasema: ”Miaka arobaini kabla.” Aadam akasema: ”Je, hukupata ndani yake:
وَعَصَىٰ آدَمُ رَبَّهُ فَغَوَىٰ
”Aadam akamuasi Mola Wake akapotoka.”[1]?
Akasema: ”Ndio.” Ndipo akasema: ”Je, unanilaumu kwa kufanya jambo ambalo Allaah aliniandikia miaka arobaini kulifanya kabla ya Yeye kuniumba?” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Aadam akamshinda Muusa.”
[1] 20:121
Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 69
Imechapishwa: 15/06/2026
Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
https://firqatunnajia.com/19-wakati-ilipoandikwa-tawraat/