Waliosema kuwa viwiliwili vya roho vilikiri kwa sura zao vilivyoumbwa kwayo
Hawshab amepokea kwamba al-Hasan amesema hivo. Kinachofahamisha kuwa Allaah (´Azza wa Jall) ndio aliwapa uwezo wa kutamka ambapo wakatamka kwa viwiliwili vyenye roho, akawapa utambuzi na ufahamu, ni yale ambayo:
35 – Ahmad bin Muhammad al-Warraaq ametukhabarisha: Muhammad bin Ismaa´iyl ametuhadithia, kutoka kwa Hajjaaj bin Muhammad, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa az-Zubayr bin Muusa, kutoka kwa Sa´iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye amesema:
”Allaah alipiga bega Lake la kulia ambapo kila nafsi iliyoumbwa kwa ajili ya Pepo ikatoka hali ya kuwa nyeupe na safi. Akasema: ”Hawa ni wakazi wa Peponi.” Kisha akapiga bega Lake la kushoto ambapo kila nafsi iliyoumbwa kwa ajili ya Moto ikatoka hali ya kuwa nyeusi.” Akasema: ”Hawa ni wakazi wa Motoni.” Kisha Akachukua kutoka kwao ahadi ya kumwamini, kumtambua, amri Yake na kumsadikisha Yeye na amri Yake kwa wanadamu wote. Akawashuhudisha juu ya nafsi zao ambapo wakasadikisha, wakatambua na kukiri.”
Nimefikiwa na khabari kwamba Aliwatoa kwenye kiganja Chake cha kuume kama punje ya hardali. Mujaahid amesimulia kutoka kwa Ibn ´Abbaas aliyesema:
”Wakati Allaah (Jalla wa ´Azz) alipowatoa alisema: ”Enyi waja Wangu, muitikieni Allaah! Uitikiaji ni utiifu.” Wakasema: ”Tunakutii, ee Allaah, tunakutii! Tumekuitikia, ee Alllaah, tumekuitikia!” Baada ya hapo Ibraahiym (´alayhis-Salaam) akapewa jumla hiyo kwenye taratibu za ´ibaadah za hijjah, nayo ni kwamba: ” Tumekuitikia, ee Alllaah, tumekuitikia!” Akapiga mgongoo wa Aadam (´alayhis-Salaam) wakati alipomuumba.”
Ibn ´Abbaas amesema:
”Alimuumba Aadam kisha Akatoa kizazi chake kutoka mgongoni mwake kama vile wadudu chungu. Akawazungumzisha kisha akawarudisha mgongoni mwake. Hakuna yeyote ambaye hakuzungumza na kusema ´Mola wangu ni Allaah`. Kila kiumbe ameumbwa na atakuwa mpaka siku ya Qiyaamah. Hayo ndio maumbile ambayo Allaah amewaumba watu kwayo.”
36 – Muslim bin al-Fadhwl ametukhabarisha huko Makkah: Muhammad bin ´Uthmaan bin Ibraahiym Abu Bilaal al-Ash´ariy ametuhadithia: Abu Bishr ametuhazdithia, kutoka kwa al-Hakam, kutoka kwa Sa´iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye amesema:
”Allaah (Jalla wa ´Azz) alimpiga bega lake la kulia – yaani la Aadam – ambapo kila nafsi iliyoumbwa kwa ajili ya Pepo ikatoka hali ya kuwa nyeupe. Akasema: ”Hawa ni wakazi wa Peponi.” Kisha akapiga bega lake la kushoto ambapo kila nafsi iliyoumbwa kwa ajili ya Moto ikatoka hali ya kuwa nyeusi.” Akasema: ”Hawa ni wakazi wa Motoni.” Kisha Akachukua kutoka kwao ahadi ya kumwamini, kumtambua na kumsadikisha. Akawashuhudisha juu ya nafsi zao ambapo wakaamini, wakasadikisha, wakatambua na kukiri.”
Wametofautiana kuhusu uitikiaji pale alipochukua fungamano kutoka kwao. Wengi wao wamesema kuwa waliitikia hali ya kutii bila ya kutenzwa nguvu. ar-Rabiy´ bin Anas amepokea kutoka kwa Abul-´Aaliyah, kutoka kwa Ubayy, ambaye amesema:
”Siku hiyo walikiri kumtii Kwake.”
Wako wanafunzi wengine wa Maswahabah pia waliosema hivo.
Wengine wamesema kuwa waliitikia umoja Wake kwa namna ya kwamba hakuna kafiri wala mwengine yeyote atakayeulizwa juu ya Mola wao, isipokuwa watasema `Mola wangu ni Allaah`.
37 – ´Aliy bin al-´Abbaas ametukhabarisha huko Gaza: Muhammad bin Hammaad ametuhadithia: ´Abdur-Razzaaq ametuhadithia, kutoka kwa Ma´mar, kutoka kwa Muhammad – kwa maana ya Ibn-us-Saa-ib –kutoka kwa Abu Swaalih, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye amesema kuhusiana na maneno Yake (Ta´ala):
وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ
“Wakati Mola wako alipochukua katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao.”
”Allaah (Jalla wa ´Azz) akapangusa mgogno wa Aadam (´alayhis-Salaam) na akatoa mgongoni mwake kizazi chake chote kitachokuwa mpaka siku ya Qiyaamah. Akachukua fungamano kwao ya kwamba Yeye ndiye Mola wao, wakampa jambo hilo. Kwa hiyo hakuna yeyote si kafiri wala mwengine atakayeulizwa ni nani Mola wake, isipokuwa atasema `Mola wangu ni Allaah`.”
as-Suddiy amesema:
”Baadhi wametii kwa khiyari yao, wengine wametii kwa kutenzwa nguvu.”
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 64-67
- Imechapishwa: 15/06/2026
- Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy

Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 64-67
Imechapishwa: 15/06/2026
Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
https://firqatunnajia.com/18-kama-wadudu-wachungu-mkononi-mwa-mola/