Waliosema kuwa walikuwa kama punje ya hardali
Twalhah bin ´Amr amepokea kutoka kwa ´Atwaa’, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye amesema:
”Aliwachukua kutoka kwenye kiganja Chake cha mkono, kama kwamba ni punje ya hardali, ya kwanaza na ya mwisho, na akawageuza kwa mkono Wake wa kuume mara mbili au mara tatu. Akiinua na kushusha mkono wake yale Anayowataka. Kisha akawarudisha mgongoni mwa baba yao mpaka alipowatoa kizazi baada ya kizazi.”
Waliosema kuwa waliitwa kwa majina yao
34 – Ahmad bin Muhammad bin Abaan ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia: Ibn Numayr ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Habiyb, kutoka kwa Sa´iyd, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye amesema:
”Allaah alitoa kizazi cha Aadam kutoka mgongoni mwake kama wadudu wachungu na akawapa majina. Akasema: ”Huyu ni fulani na huyu fulani.” Kisha Akashika kwa ngumi mbili na akasema kuambia ule mkono Wake wa kuume: ”Ingieni Peponi.” Akasema kuambia ule mkono Wake mwingine: ”Ingieni Motoni na Sijali!”
Waliosema kuwa walitolewa kama kichanuo
Mujaahid amesimulia kwamba Ibn ´Umar, ambaye amesema:
”Allaah aliwatoa kwenye mgongo wa Aadam (´alayhis-Salaam) kama kinavyotolewa kichanuo.”
Waliosema kuwa roho zilikiri kabla ya kuumbwa viwiliwili
Muusa bin ´Ubaydah ameipokea kutoka kwa Muhammad bin Ka´b al-Quradhwiy, lakini haikuthibiti.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 63-64
- Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
Waliosema kuwa walikuwa kama punje ya hardali
Twalhah bin ´Amr amepokea kutoka kwa ´Atwaa’, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye amesema:
”Aliwachukua kutoka kwenye kiganja Chake cha mkono, kama kwamba ni punje ya hardali, ya kwanaza na ya mwisho, na akawageuza kwa mkono Wake wa kuume mara mbili au mara tatu. Akiinua na kushusha mkono wake yale Anayowataka. Kisha akawarudisha mgongoni mwa baba yao mpaka alipowatoa kizazi baada ya kizazi.”
Waliosema kuwa waliitwa kwa majina yao
34 – Ahmad bin Muhammad bin Abaan ametukhabarisha: ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia: Ibn Numayr ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Habiyb, kutoka kwa Sa´iyd, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, ambaye amesema:
”Allaah alitoa kizazi cha Aadam kutoka mgongoni mwake kama wadudu wachungu na akawapa majina. Akasema: ”Huyu ni fulani na huyu fulani.” Kisha Akashika kwa ngumi mbili na akasema kuambia ule mkono Wake wa kuume: ”Ingieni Peponi.” Akasema kuambia ule mkono Wake mwingine: ”Ingieni Motoni na Sijali!”
Waliosema kuwa walitolewa kama kichanuo
Mujaahid amesimulia kwamba Ibn ´Umar, ambaye amesema:
”Allaah aliwatoa kwenye mgongo wa Aadam (´alayhis-Salaam) kama kinavyotolewa kichanuo.”
Waliosema kuwa roho zilikiri kabla ya kuumbwa viwiliwili
Muusa bin ´Ubaydah ameipokea kutoka kwa Muhammad bin Ka´b al-Quradhwiy, lakini haikuthibiti.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 63-64
Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
https://firqatunnajia.com/17-kama-punje-ya-hardali-mkononi-mwa-mola/