19. Mtume kusafirishwa mbinguni inayofahamisha ni wapi Allaah yupo

17 – Anas amesimulia kwamba Maalik bin Swa´swa´h amemweleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaeleza kuhusu safari yake aliyopandishwa mbinguni ya usiku:

“Wakati tulipokuwa karibu na kona na kwenye mlango kuna mtu alikuja kwangu… Halafu nikaletewa mnyama mweupe. Alikuwa mdogo kuliko nyumbu na mkubwa kuliko punda. Nikaketi juu yake ambapo nikaanza kwenda na Jibriyl. Wakati alipofika katika mbingu ya chini akaomba idhini ya kuingia. Kukasemwa: “Ni nani huyu?” Akasema: “Jibriyl.” Kukasemwa: “Uko pamoja na nani?” Akasema: “Muhammad.” Kukasemwa: “Je, ameitwa?” Akasema: “Ndio.” Ndipo kukasemwa: “Karibu! Neema ya mtu aliyekuja!” Ikafunguliwa na alikuwepo Aadam. Akasema: “Huyu ni baba yako Aadam. Msalimie.” Nikamsalimia na akaitikia salamu kisha akasema: “Karibu neema ya mwana mwema na Nabii mwema.”

Kisha akapandishwa mpaka akafika mbingu ya pili. Wakati alipofika akaomba idhini ya kuingia. Kukasemwa: “Ni nani huyu?” Akasema: “Jibriyl.” Kukasemwa: “Uko pamoja na nani?” Akasema: “Muhammad.” Kukasemwa: “Je, ameitwa?” Akasema: “Ndio.” Ndipo kukasemwa: “Karibu! Neema ya mtu aliyekuja!” Ikafunguliwa na hapo walikuwepo mabinamu zake Yahyaa na ´Iysaa. Akasema: “Huyu ni Yahyaa na ´Iysaa. Wasalimie.” Nikawasalimia na wakaitikia salamu kisha wakasema: “Karibu neema ya ndugu mwema na Nabii mwema.”

Halafu akapandishwa mpaka akafika mbingu ya tatu. Wakati alipofika akaomba idhini ya kuingia. Kukasemwa: “Ni nani huyu?” Akasema: “Jibriyl.” Kukasemwa: “Uko pamoja na nani?” Akasema: “Muhammad.” Kukasemwa: “Je, ameitwa?” Akasema: “Ndio.” Ndipo kukasemwa: “Karibu! Neema ya mtu aliyekuja!” Ikafunguliwa na hapo alikuwepo Yuusuf. Akasema: “Huyu ni Yuusuf. Msalimie.” Nikamsalimia na akaitikia salamu kisha akasema: “Karibu neema ya ndugu mwema na Nabii mwema.”

Kisha akapandishwa mpaka akafika mbingu ya nne. Wakati alipofika akaomba idhini ya kuingia. Kukasemwa: “Ni nani huyu?” Akasema: “Jibriyl.” Kukasemwa: “Uko pamoja na nani?” Akasema: “Muhammad.” Kukasemwa: “Je, ameitwa?” Akasema: “Ndio.” Ndipo kukasemwa: “Karibu! Neema ya mtu aliyekuja!” Ikafunguliwa na hapo alikuwepo Idriys. Akasema: “Huyu ni Idriys. Msalimie.” Nikamsalimia na akaitikia salamu kisha akasema: “Karibu neema ya ndugu mwema na Nabii mwema.”

Kisha akapandishwa mpaka akafika mbingu ya tano. Wakati alipofika akaomba idhini ya kuingia. Kukasemwa: “Ni nani huyu?” Akasema: “Jibriyl.” Kukasemwa: “Uko pamoja na nani?” Akasema: “Muhammad.” Kukasemwa: “Je, ameitwa?” Akasema: “Ndio.” Ndipo kukasemwa: “Karibu! Neema ya mtu aliyekuja!” Ikafunguliwa na hapo alikuwepo Haaruun. Akasema: “Huyu ni Haaruun. Msalimie.” Nikamsalimia na akaitikia salamu kisha akasema: “Karibu neema ya ndugu mwema na Nabii mwema.”

Halafu akapandishwa mpaka akafika mbingu ya sita. Wakati alipofika akaomba idhini ya kuingia. Kukasemwa: “Ni nani huyu?” Akasema: “Jibriyl.” Kukasemwa: “Uko pamoja na nani?” Akasema: “Muhammad.” Kukasemwa: “Je, ameitwa?” Akasema: “Ndio.” Ndipo kukasemwa: “Karibu! Neema ya mtu aliyekuja!” Ikafunguliwa na hapo alikuwepo Muusa. Akasema: “Huyu ni Muusa. Msalimie.” Nikamsalimia na akaitikia salamu kisha akasema: “Karibu neema ya ndugu mwema na Nabii mwema.” Nilipompita nikaanza kulia. Akaulizwa: “Kipi kinachokuliza?” Akasema: “Nalia kwa sababu ya kijana aliyetumwa baada yangu aliye na Ummah ambao watu wake wengi wataingia Peponi kuliko Ummah wangu.”

Kisha akapandishwa mpaka akafika mbingu ya saba. Wakati alipofika akaomba idhini ya kuingia. Kukasemwa: “Ni nani huyu?” Akasema: “Jibriyl.” Kukasemwa: “Uko pamoja na nani?” Akasema: “Muhammad.” Kukasemwa: “Je, ameitwa?” Akasema: “Ndio.” Ndipo kukasemwa: “Karibu! Neema ya mtu aliyekuja!” Ikafunguliwa na hapo alikuwepo Ibraahiym. Akasema: “Huyu ni Ibraahiym. Msalimie.” Nikamsalimia na akaitikia salamu kisha akasema: “Karibu neema ya mwana mwema na Nabii mwema.”

Halafu akapandishwa mpaka kwenye mkunazi wa mwisho kabisa. Halafu nikanyanyuliwa Nyumba yenye kuamrishwa. Halafu nikafaradhishiwa swalah khamsini kila siku. Nilipokuwa njiani narudi nikakutana na Muusa ambaye akasema: “Umefaradhishiwa nini?” Nikasema: “Nimefaradhishiwa swalah khamsini kwa siku.” Akasema: “Ummah wako hauwezi swalah khamsini. Mimi nimewajaribu watu kabla yako na nimetangamana na wana wa Israa´iyl kwa ukali kabisa. Hivyo rudi kwa Mola wako na umuombe akupunguzie.” Nikarudi na nikapunguziwa kumi.

Nikarudi kwa Muusa ambapo akasema: “Umefaradhishiwa nini?” Nikasema: “Nimefaradhishiwa swalah arubaini kwa siku.” Akasema: “Ummah wako hauwezi swalah arubaini. Mimi nimewajaribu watu kabla yako na nimetangamana na wana wa Israa´iyl kwa ukali kabisa. Hivyo rudi kwa Mola wako na umuombe akupunguzie.” Nikarudi na nikapunguziwa tena kumi.

Nikarudi tena kwa Muusa ambapo akasema: “Umefaradhishiwa nini?” Nikasema: “Nimefaradhishiwa swalah thelathini kwa siku.” Akasema: “Ummah wako hauwezi swalah thelathini. Mimi nimewajaribu watu kabla yako na nimetangamana na wana wa Israa´iyl kwa ukali kabisa. Hivyo rudi kwa Mola wako na umuombe akupunguzie.” Nikarudi na nikapunguziwa tena kumi.

Nikarudi tena kwa Muusa ambapo akasema: “Umefaradhishiwa nini?” Nikasema: “Nimefaradhishiwa swalah ishirini kwa siku.” Akasema: “Ummah wako hauwezi swalah ishirini. Mimi nimewajaribu watu kabla yako na nimetangamana na wana wa Israa´iyl kwa ukali kabisa. Hivyo rudi kwa Mola wako na umuombe akupunguzie.” Nikarudi na nikapunguziwa tena kumi.

Nikarudi tena kwa Muusa ambapo akasema: “Umefaradhishiwa nini?” Nikasema: “Nimefaradhishiwa swalah kumi kwa siku.” Akasema: “Ummah wako hauwezi swalah kumi. Mimi nimewajaribu watu kabla yako na nimetangamana na wana wa Israa´iyl kwa ukali kabisa. Hivyo rudi kwa Mola wako na umuombe akupunguzie.” Nikarudi na nikapunguziwa tena kumi.

Nikarudi tena kwa Muusa ambapo akasema: “Umefaradhishiwa nini?” Nikasema: “Nimefaradhishiwa swalah tano kwa siku.” Akasema: “Ummah wako hauwezi swalah tano. Mimi nimewajaribu watu kabla yako na nimetangamana na wana wa Israa´iyl kwa ukali kabisa. Hivyo rudi kwa Mola wako na umuombe akupunguzie.” Nikarudi na nikapunguziwa tena kumi.”

Nimemuomba Mola wangu sana mpaka nikaona haya. Mimi naridhia na najisalimisha. Baada ya hapo akanadi mwenye kunadi: “Nimetekeleza faradhi Yangu na nimewasahilishia waja Wangu.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

[1] al-Bukhaariy (3887) na Muslim (162). Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) ametaja katika “Ijtimaa´-ul-Juyuush al-Islaamiyyah”, uk. 29, ya kwamba Hadiyth inayozungumzia safari ya kupandishwa mbinguni imepokelewa kwa njia nyingi. Haafidhw Ibn Kathiyr amekusanya nyingi katika njia zake na baadaye as-Suyuutwiy akazifupisha katika kitabu chake “al-Aayaat al-Kubraa fiyl-Mi´raaj wal-Israa””. Hapana shaka ya kwamba msingi wa kisa umepokelewa kupitia njia tele. Kuhusu upambanuzi wake, kuna sehemu kubwa ambayo ni Swahiyh na nyingine kinyume na hivo.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 88-89
  • Imechapishwa: 12/04/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy