18. Wakati Mtume alipoingia kwa Mola wake

16 – Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Nitaingia kwa Mola wangu (´Azza wa Jall) wakati Yuko juu ya ´Arshi Yake (Tabaarak wa Ta´ala).”

Zaaidah ni mnyonge. Mfano wa Hadiyth yenyewe iko katika ”as-Swahiyh”[1] ya al-Bukhaariy kupitia kwa Qataadah, kutoka kwa Anas, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

”Nitamuomba idhini Mola wangu ya kumwendea katika makazi Yake, ambapo atanipa idhini.”

Ameipokea al-´Assaal katika ”Kitaab-ul-Ma´rifah” kwa cheni ya wapokezi yenye nguvu kupitia kwa Thaabit, kutoka kwa Anas na ndani yake kuna:

”Nitafika kwenye mlango wa Peponi ambapo nitafunguliwa nao. Nimwendee Mola wangu ilihali Yuko juu ya Kursiy Yake, ambapo nitaporomoka chini kumsujudia.”

[1] Hata hivyo ameipokea kwa cheni ya wapokezi pungufu. Mtunzi ameipokea Hadiyth katika toleo la asili. Hata hivyo sentesi isemayo ”katika makazi Yake” ni dhaifu, kama nilivyolibainishia katika taaliki yangu ya ”Mukhtaswar Swahiyh al-Bukhaariy” mwanzoni mwa ”Kitaab-ut-Tawhiyd”. Aidha Hadiyth imepokelewa kupitia kwa Thaabit, kutoka kwa Anas kupitia kwa njia nyingine na itakuja huko mbele kwenye kitabu. ad-Daarimiy amepokea mfano wake katika  “ar-Radd ´alaal-Mariysiy”, uk. 14, na Ahmad kupitia kwa Ibn ´Abbaas. Abu Ja´far ameipokea katika ”al-´Arsh” (1/113 – muswada). Inatiliwa nguvu pia na Hadiyth nyingine ndefu kuhusu Mkusanyiko iliopokelewa na Abu Hurayrah na inapatikana katika ”al-´Adhwamah” (1/66 na 1/72 – muswada) ya Abush-Shaykh.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 87-88
  • Imechapishwa: 12/04/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy