17. Hukumu ya Mfalme kutoka juu ya mbingu ya saba

15 – Sa´d bin Abiy Waqqaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia Sa´d bin Mu´aadh (Radhiya Allaahu ´anhumaa):

”Umewahukumu kwa hukumu ya Mfalme kutoka juu ya mbingu ya saba.”[1]

Swahiyh na ameipokea an-Nasaa´iy.

[1] Ameipokea pia al-Bayhaqiy katika ”al-Asmaa´ was-Swifaat”, uk. 420, na cheni ya wapokezi wake ni nzuri. Humo yuko Muhammad bin Swaalih at-Tammaar ambaye Haafidhw Ibn Hajar amesema juu yake:

”Ni mkweli anayekosea.”

adh-Dhahabiy amemtaja katika ”Miyzaan-ul-I´tidaal” ambapo ametaja makinzano ya maimamu juu yake. Hata hivyo Hadiyth ina nyingine inayoitia nguvu katika ´Alqamah bin Waqqaasw, pasi na Swahabah katika cheni ya wapokezi. Kwa mujibu wa ”Fath-ul-Baariy” ameipokea Ibn Ishaaq. Mtunzi ameitaja katika toleo la asili kupitia kwa Muhammad bin Maalik ambapo amesema kuwa kuna Swahabah anayekosekana katika cheni ya wapokezi. Hata hivyo Hadiyth imepokelewa katika al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) kwa kifupi.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 87
  • Imechapishwa: 12/04/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy