16. Swadaqah pekee inayopanda kwa Allaah

14 – Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah hukubali swadaqah ya mja kutoka katika chumo zuri – na hakuna anachokubali Allaah isipokuwa kilicho kizuri na hakuna kinachopanda Kwake isipokuwa kilicho kizuri; anaichukua tende na kuilea mpaka inakuwa kama mlima.”

Swahiyh[1].

[1] Mambo ni kama alivosema. Cheni ya wapokekezi ya mtunzi katika toleo la asili ni Swahiyh, lakini siwezi kuiona katika yale marejeo mengine kupitia kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy. Hata hivyo inapatikana kwa maana kama hiyo kwa al-Bukhaariy na Muslim na wengineo kupitia kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – imekwishatajwa katika nambari 11. Ahmad ameipokea kupitia njia nyingi – (2/268, 328, 404, 418, 431, 528 na 541). Ibn Abiy ´Aaswim ameipokea katika “as-Sunnah” (824).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 86-87
  • Imechapishwa: 12/04/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy