15. Namna hii hupanda kwa Allaah du´aa aliyedhulumiwa

13 – Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Iogopeni du´aa ya mwenye kudhulumiwa; hakika hupanda kwa Allaah kana kwamba ni cheche.”[1]

Geni. Cheni ya wapokezi wake ni nzuri.

[1] Ameipokea al-Haakim na wengineo, kama nilivyolibainisha katika “Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah” (869).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 86
  • Imechapishwa: 12/04/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy