14. Matendo yanapandishwa juu kwa Allaah

12 – Abu Muusa al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah halali na wala haimstahikii Yeye kulala. Anaishusha mizani na kuinyanyua. Kwake kunapandishwa matendo ya usiku kabla ya mchana na matendo ya mchana kabla ya usiku. Pazia Yake ni Nuru; lau ataifunua, basi mwanga wa uso Wake ungeliunguza kila anachoona katika uumbaji Wake.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

[1] Muslim (179).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 86
  • Imechapishwa: 12/04/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy