13. Chumo zuri pekee ndilo linalopanda kwa Allaah

11 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule anayetoa swadaqah sawa na tende kutoka katika pato zuri – na wala hakuna kinachopanda kwa Allaah isipokuwa kilicho kizuri – isipokuwa Allaah anaipokea kwenye mkono Wake wa kuume na anailea kama anavyolea mmoja wenu kitekli chake ambapo tende inakuwa kama mlima mkubwa.”[1]

Hadiyth hii ni Swahiyh na ameipokea al-Bukhaariy.

[1] al-Bukhaariy (7430).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 86
  • Imechapishwa: 12/04/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy