12. Wakati Muusa alipompiga Malaika wa mauti

10 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Malaika wa kifo alikuwa akiwajia watu hali ya kuonekana. Akamjia Muusa (´alayhis-Salaam) ambapo akampiga na jicho lake likatoka. Hivyo akapanda kwa Mola wake (´Azza wa Jall) akasema: ”Ee Mola! Umenituma kwa Muusa ambaye amenipiga na jicho langu limetoka. Kama isingelikuwa nafasi yake mbele Yako, basi ningemfanyia uzito.” Akasema: ”Rejea kwa mja Wangu na umwambie aweke wake juu ya fahali; atapata mwaka kwa kila unywele uliyoguswa na mkono wake.” Akamwendea na kumweleza kile alichoamrishwa. Akasema: ”Kisha nini kitatokea baada ya hapo?” Akajibu: ”Kufa.” Akasema: ”Basi chukua hivi sasa.” Akamfanya kunusa harufu ambapo akachukua roho yake; na Allaah akamrudishia Malaika wa mauti macho yake.”

Imekuja katika tamko jingine:

”Malaika wa mauti akamwendea Muusa bin ´Imraan (´alayhis-Salaam) na akamwambia: ”Mwitikie Mola wako!” Muusa (´alayhis-Salaam) akampiga Malaika wa kifo ambapo likaondoka. Malaika wa kifo akarudi kwa Allaah (Ta´ala) na kusema: ”Umenituma kwa mja asiyetaka kufa. Amenipiga jicho langu.” Allaah akamrudishia jicho lake na akasema: ”Rejea kwa mja Wangu na umwambie aweke wake juu ya fahali; atapata mwaka kwa kila unywele uliyoguswa na mkono wake.” Akamwendea na kumweleza kile alichoamrishwa. Akasema: ”Kisha nini kitatokea baada ya hapo?” Akajibu: ”Kufa.” Akasema: ”Basi chukua hivi sasa. Ee Mola wangu! Nisogeze karibu na ardhi Takatifu!” Naapa kwa Allaah! Iwapo ningekuweko hapo basi ningekuonyesheni kaburi lake karibu na njia ya duna nyekundu.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim[1].

[1] Hivi ndivo imekuja katika ”muswada” na katika machapisho yote, jambo ambalo linatakiwa kuangaliwa vyema. Kwa sababu hakuna yeyote aliyepokea tamko la kwanza. Mambo yalivyo ni kuwa ameipokea Ahmad (02/533) kwa cheni ya wapokezi nzuri. Kadhalika amepokea tamko mfano wa hilo kupitia njia zingine: (2/269), (2/310) na (2/351). Imetajwa katika ”Dhwilaal-ul-Jannah fiy Takhriyj-is-Sunnah” (801-802). Ibn-ul-Qayyim alikuwa makini zaidi wakati alipotaka vyanzo vya Hadiyth kuliko mtunzi na akasema:

”Hadiyth ni Swahiyh. Msingi na mapokezi yanayoitia nguvu yanapatikana kwa al-Bukhaariy na Muslim.” (Ijtimaa´-ul-Juyuush al-Islaamiyyah, uk. 37).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 85-86
  • Imechapishwa: 12/04/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy